• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda na China kukuza zaidi ushirikiano

    (GMT+08:00) 2017-07-31 20:06:23

     

    Balozi wa China nchini Rwanda Rao Hongwei amesema kampuni zaidi za China hivi karibuni zitawekeza nchini humo.

    Aidha balozi huyo amesema watalii zaidi wa China watatembelea Rwanda hali ambayo natarajiwa kukuza uchumi wanchi hiyo.

    Alisema kufuatia hazina ya dola milioni 10 ilioazishwa na mfanya biashara maarufu wa China Jack Ma wajasiriamali vijana nchini Rwanda watanufaika .

    Rwanda ikiwa na uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki, inaendelea kuimarisha biashara kati yake na China sana sana kwenye sekta za ununuzi wa bidhaa na uwekezaji.

    Mapema mwaka huu rais wa Rwanda Paul Kagame, alifanya ziara nchini China ambapo alikutana na mwenyeji wake rais wa China Xi Jinping na kukubaliana kukuza ushirikiano wenye utafaidi Kigali na Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako