• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na Kampuni ya Barrick kuanza mazungumzo kuhusu mgogoro wa uchimbaji dhahabu

    (GMT+08:00) 2017-08-01 09:31:42

    Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold, inayomiliki hisa nyingi kwenye kampuni ya Acacia, wameanza mazungumzo ya kutaka kukomesha mgogoro wa muda mrefu kuhusu malipo inayodaiwa kampuni hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania mjini Dar es salaam, inasema mazungumzo hayo yanafanyika kati ya tume maalum inayoongozwa na waziri wa sheria na katiba wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi, na mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Bw Richard Williams.

    Mazungumzo hayo yanafuatia mazungumzo kati ya Rais John Magufuli wa Tanzania na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Profesa John Thompson mjini Dar es salaam.

    Tarehe 21 mwezi huu, Rais John Magufuli alisema kuwa atafunga migodi hiyo kama mazungumzo kuhusu malimbikizo ya malipo yatacheleweshwa. Wiki iliyopita serikali ya Tanzania ilitangaza kuidai kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia jumla ya dola za kimarekani bilioni 190, ambazo ni kodi na adhabu za kutolipa kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako