• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yabadilisha kanuni nane za Ligi kuimarisha mchezo

    (GMT+08:00) 2017-08-01 10:31:48

    Siku chache kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara 2017/2018, Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya Bodi ya Ligi, limetangaza mabadiliko mapya kuimarisha mchezo.

    Afisa wa habari wa shirikisho hilo Alfred Lucas amesema kuwa kuna mabadiliko ya kanuni nane ambazo zimefanyiwa marekebisho baada ya kamati ya Bodi ya Ligi kukutana na viongozi wa vilabu zinazoshiriki Ligu kuu Tanzania.

    Lucas amefichua kuwa mkutano huo ulifanyika wiki iliyopita ajenda kuu ikiwa kujadili uchaguzi ujao wa TFF na mapendekezo ya kurekebishwa kwa kanuni za Ligi Kuu. Kulingana na taarifa yake kanuni zilizoguswa zaidi ni kanuni ya 18 inayohusu Bima kwa wachezaji.

    Kwenye kanuni mpya, kila klabu inatakiwa kuwawekea wachezaji wake bima ya matibabu na fidia kutokana na ajali michezoni. Klabu itakayokiuka kanuni hii haitapata leseni kuendesha shughuli zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako