• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makocha wa Nyumbani kuiongoza Cranes

    (GMT+08:00) 2017-08-01 10:32:08

    Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA sasa limetangaza kuwa makocha wa nyumbani Moses Basena na Fred Kajoba watashika usukunani na kuiongoza timu ya taifa ya Kandanda Uganda Cranes katika mechi zote ambazo timu hiyo imeratibiwa kucheza.

    Rais wa FUFA Moses Magogo amefichua kuwa itakuwa vigumu kupata kocha mpya kwa haraka kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mserbia Micho Sredojevic aliyegura timu hiyo wikendi hii.

    Magogo alikiri kuwa kuondoka kwa Micho ni Pigo kwa Uganda lakini akasisitiza kuwa timu hiyo lazima iendelee mbele. Kwa sababu hii, Rais huyo amesema Basena na Kajoba wataifunza timu hiyo kwa muda hadi pale usaili utafanywa kwa ajili ya kocha mpya atakayejaza pengo lililopo kwa sasa.

    Magogo anasema wawili hao wana uzoefu wa kutosha na kwamba shirikisho lake lina Imani watafanya vyema. Kibarua ya kwanza ya makocha hao wa nyumbani itakuwa kuiongoza Cranes katika mechi ya kufuzu CHAN dhidi ya Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako