• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Voliboli ya Rwanda yakosa kufuzu Kombe la Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-08-01 10:32:48

    Timu ya taifa ya wanawake ya voliboli ya Rwanda ilikosa kujikatia tikiti ya kuingia mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu baada ya kupoteza mechi zake zote tatu katika mashindano ya CAVB Zone V Championships yaliyokamilika jijini Nairobi.

    Mashindano hayo ya bara yameratibiwa kuanza Octoba 7 hadi 14 katika mji mkuu wa Cameroon Yaounde.

    Timu hiyo inayoonzwa na kocha Jean Marie Nsengiyumva ilikosa kusajili ushindi hata mmoja katika mechi zake zote baada ya kushindwa na Uganda 2-3, Misri 3-1 kabla ya kulamba sakafu dhidi ya wenyeji Kenya 3-0.

    Kenya ilimaliza ya kwanza katika mashindano hayo ya timu nne ikiwa na pointi 9, mbele ya Misri iliyomaliza ya pili ilhali Uganda ilifuzu nambari ya tatu na pointi tatu na Rwanda kufuta mkia ikiwa na pointi moja pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako