• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nemanja Matic hatimaye amejiunga na Man Utd

  (GMT+08:00) 2017-08-01 10:33:06

  Manchester United wamekamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kutoka kwa mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea kwa milioni 40 pauni ya Uingereza.

  Matic mwenye umri wa miaka 28 ametia saini mkataba wa miaka mitatu na kuwa mchezaji wa tatu kasajiliwa na Manchester United katika kipindi hiki cha uamisho.

  Kocha mkuu wa Manchester United Jose Mourinho alisifu hatua ya kumsajili Matic akimtaja kama mchezaji anayecheza vyema na wenzake kwenye timu huku Matic akisema ana furaha sana kujiunga na United wakati huu wa kusisimua.

  Itakumbukwa kwamba kocha Mourinho, alimnunua Matic kuingia Chelsea, kutoka klabu ya Benfica Januari 2014.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako