• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China asisistiza kushikilia njia ya kujenga jeshi lenye nguvu kubwa iliyo na umaalumu wa China

  (GMT+08:00) 2017-08-01 16:54:52

  Mkutano wa kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi la umma la China PLA umefanyika leo hapa Beijing, rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano huo na kusisitiza kuwa, ili kutimiza ustawi wa China na maisha mazuri zaidi kwa wachina, ni lazima kulijenga jeshi la China kuwa na nguvu kubwa duniani. Pia amesema China itashikilia njia ya kuimarisha uwezo wa jeshi kwa umaalumu wa China.

  Rais Xi Jinping amesema, ni lazima kushikilia uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China kwa jeshi la umma bila kulega, kuhakikisha jeshi la umma linafuata Chama cha Kikomunisti cha China daima, kuinua kiwango cha kisasa wa ulinzi wa taifa na jeshi la umma, kuhimiza maendeleo ya mafungamano kati ya jeshi na raia, na kushikilia nia ya kimsingi ya kuwahudumia umma, na kujenga jeshi linaloaminiwa na kupendwa na wananchi.

  Rais Xi Jinping amesema, China siku zote ni mjenga wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, na mlinzi wa utaratibu wa kimataifa, na jeshi la China ni nguvu muhimu ya kulinda amani ya dunia. Amesisitiza kuwa, wananchi wa China wanapenda amani, China haitavamia nchi nyingine siku zote, lakini ina imani ya kushinda uvamizi wowote.

  Rais Xi Jinping pia amesema, China haitaruhusu mtu yoyote, makundi yoyote na chama chochote kutenga ardhi yoyote kutoka China kwa njia yoyote na wakati wowote.

  Ameongeza kuwa China haitavumilia kuharibika kwa mamlaka ya taifa, usalama wa nchi na maslahi ya maendeleo. Rais Xi pia amesisitiza kuwa, jeshi la ukombozi la umma la China lazima lilinde uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na utaratibu wa kijamii, kulinda mamlaka ya taifa, usalama na maendeleo ya China, na kulinda amani ya kikanda na ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako