• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa uchumi na biashara wa nchi za BRICS wafunguliwa mjini Shanghai

    (GMT+08:00) 2017-08-01 18:34:28

    Mkutano wa mawaziri wa uchumi na biashara wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) umefunguliwa leo mjini Shanghai. Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan amesema, mkutano huo utatilia mkazo masuala mbalimbali yakiwemo kurahisisha uwekezaji, kusukuma mbele biashara, kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia, na kuunga mkono mfumo wa biashara kati ya pande nyingi.

    Bw. Zhong amesema uchumi wa dunia umefufuka katika miaka kadhaa iliyopita, lakini bado unakabiliwa na changamnoto mbalimbali. Amesema nchi za BRICS zinatakiwa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kuboresha utaratibu wa kushirikiana, kupanua sekta za ushirikiano, kutunga hatua mpya za ushirikiano, na kutafuta injini mpya ya maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako