• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda kuongeza juhudi kuboresha chai yake

    (GMT+08:00) 2017-08-01 19:20:28

    Halmashauri ya kuuza bidhaa za kilimo nje nchini Rwanda

    (NAEB) inaongeza juhudi za kuongeza mauzo ya chai.

    Maneja wa kitengo cha mauzo ya chai kwenye halmashauri hiyo Issa Nkurunziza, anasema wameanzisha mikakati mipya ya kupunguza gharama na kuhakikisha ubora wa majani unadumishwa.

    Aidha halmashauri hiyo inaendelea kusaidia mikakati ya kupanua maeneo yanayopandwa chai.

    Nkurunziza amesema pia wanawahimiza wakaazi wa Rwanda kunywa chai kwa wingi na kusaidia kuifanya bidhaa hiyo kutambuliwa kote duniani.

    Mahitaji ya chai ya Rwanda kulingana na taakwimu yalipanda wiki iliopita ambapo iliuza vifurushi 136,100 ikilinganishwa na 123,784 kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako