• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Safari za ndege Kenya zarejelea hali ya kawaida

    (GMT+08:00) 2017-08-01 19:20:56

    Shirika la ndege nchini Kenya Kenya Airways lilifuta safari zake Jumatatu baada ya marubani kukataa kuendeesha baadhi ya ndege.

    Shirika hilo pia lilifuta safari zake kadhaa wikendi kufuatia mgomo wa marubani.

    Hata hivyo sasa safari zimerejelea hali ya kawaida.

    Bado haijabainika kwa nini wanafanya mgomo huo lakini mwaka jana waligoma wakimtaka mwenyekiti wa halmashauri wake Mbuvi Ngunze kuondoka.

    Nafasi ya Ngunze hivi karibuni ilichukuliwa na Sebastian Mikosz, ambaye awali alikuwa mkurungezi wa shirika la ndege la Poland.

    Jumamosi hii shirika hilo lilifuta safari 8 zizizotarajiwa kuondoka kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

    Sasa linasema shirika hilo kwamba limeanza mchakato wa kusuluhisha tatatizo lililopo na marubani na kuepusha hali kama hiyo.

    Shirika hilo bado linakabiliwa na hasara na matatizo ya kifedha, mwezi Machi mwaka huu likiwa na hasara ya shilingi bilioni 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako