• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi dhidi ya maafisa wa TFF na Simba yahairishwa

    (GMT+08:00) 2017-08-02 10:33:20

    Upande wa mashtaka jana iliomba mahakama iliyoko Dar es Salaam kutoa muda zaidi kuwawezesha kukamilisha uchunguzi kuhusiana na madai ya ufisadi dhidi ya maafisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushirikiano na wasimamizi wa Simba Sports Club.

    Katika kesi inayomkabili Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu Mwesigwa Selestine na mhasibu wa shirikisho hilo Nsiande Mwanga, wakili wa serikali Nassoro Katuga, alimuharifu hakimu Mkazi Wilbard Mashauri kwamba uchunguzi kuhusiana na kesi zao bado ulikuwa haujakamilika

    Maombi kama hayo yalitolewa na mkuu wa mashtaka kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa PCCB kwa kesi inayowakabili wakuu wa Simba. Kwa kesi zote mbili, mahakimu walikubaliana na maombi ya ofisi za mashtaka na kuahirisha kesi hizo hadi Agosti 7 na 11. Hata hivyo wakili wa washtakiwa alielezea kutoridhishwa kwake na kasi ya kesi hizo na akaomba upande wa mashtaka kuharakisha mchakato huo ili wateja wake wajue hatima yao

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako