• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanariadha wa Uganda walalamikia kukosekana kwa Kipsiro na Kiprotich

    (GMT+08:00) 2017-08-02 10:33:48

    Wanariadha wa masafa marefu kutoka Uganda Stephen Kiprotich na Moses Kipsiro hawatashiriki katika mashindano ya dunia yatakayoanza karibuni jijini London, Uingereza.

    Wawili hao watakosa mashindano hayo baada ya kuomba kutoshirikishwa wakidai hawako katika hali nzuri ya kushindana na wapinzani wao. Hatua hii hata hivyo haijapokelewa vyema na wanariadha chipukizi kutoka Uganda.

    Kizazi cha sasa cha wanariadha kutoka Uganda wamekuwa wakiwatazamia wawili hao kuwatia moyo kwa sababu ya uzoefu wao wa zaidi ya miaka 15. Kipsiro na Kiprotich wameshinda jumla ya medali 6 ya jumuia ya madola, Olimpiki na mbio za dunia.

    Japo shirikisho la riadha nchini Uganda imewasihi wawili hao kubadili nia yao ya kutoshiriki mashindano ya London, Kipsiro na Kiprotich wanasisitiza kuwa hilo halitawezekana kwa sasa.

    Kulingana na shirikisho hilo Uganda itakosa uzoefu na uongozi katika mashindano hayo. Aidha kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo kimekiri kitawakosa kwani kipsiro na Kiprotich wamekuwa wakiwapa msukumo kufanya vyema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako