• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bolt aonya dhidi ya matumizi ya dawa ya kusisimua misuli

  (GMT+08:00) 2017-08-02 10:34:44

  Mwanariadha mahiri kutoka Jamaica Usain Bolt anasema wanariadha ambao wanatumia dawa za kusisimua misuli lazima waache tabia hiyo kwani inahatarisha maisha yao na michezo kwa jumla. Bolt anadai kuwa taaluma ya michezo kwa sasa inakabiliwa na tishio kubwa kutoka matumizi ya dawa hizo.

  Bolt anayepanga kukimbia mbio ya mwisho katika taaluma yake iliyojaa mafanikio, anasema anahofu hatima ya riadha iwapo tabia hii itaruhusiwa kuendelea. Anasema ni maombi yake makubwa kwamba wanariadha wenzake watasaidia juhudi za kusaidia michezo kusonga mbele wala sio nyuma kwa sababu ya kutumia njia haramu kujipatia umaarufu.

  Bolt mwenye umri wa miaka 30 amekiri kuwa madai yaliyotolewa hivi karibuni kwenye ripoti ya McLaren kuhusu matumizi ya madawa hizo kwa msaada kutoka watu fulani nchini Russia ni la kuhuzunisha na imeiletea taaluma hiyo sifa mbaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako