• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano manane ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara yasainiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa nchi za BRICS

    (GMT+08:00) 2017-08-02 17:42:32

    Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan leo ametangaza kuwa, Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zimefikia maoni ya pamoja kwenye pande nane zikiwemo kupitisha mpango wa ushirikiano wa biashara ya huduma kati yao, mpango wa ushirikiano wa kurahisisha uwekezaji na mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi.

    Mkutano huu ni mkutano wa kwanza wa mawaziri wa uchumi na biashara, baada ya ushirikiano kati ya nchi za BRICS kuingia kwenye kipindi cha pili cha miaka kumi. Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan amesema, mpango wa ushirikiano wa kurahisisha uwekezaji ni waraka maalumu wa kwanza kwenye eneo la kurahisisha uwekezaji duniani. Amesema mpango huo umeeleza mifano mizuri ya uwekezaji ya nchi za BRICS, utazisaidia nchi hizo zifanye mfumo wa uwekezaji uwe wazi zaidi, kuongeza ufanisi wa utaratibu wa kiserikali unaohusiana na uwekezaji, kuinua kiwango cha huduma za uwekezaji, kuweka mazingira ya sera yanayonufaisha uwekezaji, na kutilia mkazo kutimiza maendeleo endelevu ya nchi za BRICS.

    Hivi sasa biashara ya kielektroniki imekuwa shughuli ya biashara zenye nguvu ya uhai zaidi. Mawaziri wa uchumi na biashara wamepitisha kwa pamoja "Pendekezo la ushirikiano kati ya nchi za BRICS kwenye biashara ya elektroniki", ili kuhimmiza ongezeko la biashara, kufanya marekebisho ya miundo ya viwanda, na kuzisaidia nchi zinazoendelea na kampuni ndogo zinufaike na maendeleo ya dunia.

    Bw. Zhong Shan amesema baada ya muda mfupi, wachina wanaweza kuona bidhaa zenye umaalumu kutoka nchi za BRICS, na kampuni za China pia zitafanya ushirikiano na kampuni za nchi nyingine za BRICS kwenye uuzaji kwa njia ya biashara ya elektroniki, usafirishaji wa bidhaa, na njia ya kulipa.

    Licha ya hayo, nchi hizo tano zimefikia maoni ya pamoja kuhusu kuunga mkono utaratibu wa biashara unaoshirikisha pande zote, na kupinga shughuli za kujilinda kibiashara. Vilevile zimekaribisha kufanyika mwaka kesho kwa maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako