Kampuni moja ya China itasaidia Uganda kupata mabaki ya meli ya mizigo iliozama mwaka wa 2005 katika ziwa victoria.
Kampuni hiyo ya Tianjin Dredging itatumia dola miliooni 500 kwa kazi hiyo na pia kuwekeza kwenye sekta ya maji nchini humo.
Kampuni hiyo pia inatarajiwa kujenga meli ya abiria itakayohudumu kwenye ziwa hilo na mengineyo ili kuinua uchumi na utalii wa Uganda.
Meneja wa kampuni hiyo Jiang Xinbiao, amekutana na ujumbe wa rais Yoweri
Museveni mjini Tianjin wiki iliopita ambapo walikubaliana kwamba ofisi ya kampuni hiyo ilioko mjini Nairobi itahamishwa mjini Kampala ili kurahisisha mawasiliano yanayohusiana na uwekezaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |