• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wenye hoteli Uganda washinikiza serikali kuwapunguzia ushuru

    (GMT+08:00) 2017-08-02 19:12:19

    Wenye hoteli nchini Uganda wanaendelea kuishinikiza serikali kupunguza ushuru kwao wakisema kwamba sasa watalii wamepungua huku gharama za oparesheni zikipanda.

    Awali bunge nchini humo lilipinga pendekezo la wenye hoteli kwamba wapunguziwe asilimia 18 ya ushuru hasa kwa hoteli zilizoko nje ya mji mkuu Kampala.

    Mwenyekiti wa chama cha wenye hoteli nchini humo Susan Muhwezi, amesema hoteli nyingi zimesalia bila wageni kwa miezi kadhaa ya mwaka huu lakini wakati huo huo wanahitajika kulipa bili za maji, umeme na mishahara.

    Takwimu za chama hicho zinaonyesha kwamba hoteli zilizoko nje ya kampala zinapata wageni kwa asilimia 30 tu huku nazo nyumba za malazi kwenye hifadhi za wanyama zikipata asilimia 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako