• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yateua wanachama wapya kamati ya LAC

    (GMT+08:00) 2017-08-03 10:29:10
    Zikiwa zimesalia siku 25 pekee kabla ya kuanza kwa lugi kuu ya bara nchini Tanzania, shirikisho la soka nchini humo TFF imewateua wanachama wapya wa kamati yake ya kutoa leseni kwa vilabu.

    Kulingana na taarifa kutoka TFF, kamati ya utendakazi ya shirikisho hilo lilikutana karibuni na kumteua wakili Damas Ndumbaro kama mwenyekiti wa kamati hiyo.

    Ndumbaro anarejea kwenye wadhifa huo baada ya kamati ya nidhamu ya TFF kuondoa marufuku hivi majuzi iliyokuwa imemwekea. Sasa Ndumbaro atasaidiwa na wakili Alex Mgongolwa.

    Kamati hiyo inajukumu la kushughulikia rufaa kutokana na maamuzi yanayofanywa na kamati ya kutoa leseni kwa vilabu. Kulingana na kanuni mpya, vilabu vyote vinavyoshiriki daraja ya juu, vinahitajika kutuma maombi ya kupewa leseni mpya kwa muda ambao umetangazwa na kamati ya utendakazi ya TFF.

    Aidha vilabu hivyo vinatakikana kuhakikisha kuwa vimeitimu mahitaji yote ili kupokea leseni hiyo ya kushiriki ligi, la sivyo vitashushwa daraja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako