• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama yaruhusu Nock kuandaa uchanguzi wake

    (GMT+08:00) 2017-08-03 10:29:32
    Kamati ya kitaifa ya Olimpiki ya Kenya NOCK sasa imepewa ruhusa kuandaa uchaguzi wake kulingana na agizo lililotolewa na mahakama siku ya Jumatano.

    Jaji Enock Chacha Mwita aliweka kando agizo lililozuia uchaguzi huo kufanyika kupitia ombi la chama cha Taekwondo ya Kenya KTA mwezi mei mwaka huu.

    Jaji Mwita alitoa uamuzi huo baada ya pande zote kukosa kuafikiana nje ya mahakama kama ilivyoagizwa na mahakama hiyo siku ya jumatatu.

    Jaji huyo aliamuru kufanyika kwa uchaguzi huo kwani agizo lililokuwa limesimamisha shughuli hiyo imeondolewa.

    Wadau wa riadha nchini Kenya walikuwa wamehofu kwamba iwapo NOCK ingeshindwa kuandaa uchaguzi huo, basi nchi hiyo ingepigwa marufuku na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, IOC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako