• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha mpira wa vikapu ya Rwanda yatajwa

    (GMT+08:00) 2017-08-03 10:30:17
    Kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa vikapu ya Rwanda Moise Mutokambali ametaja kikosi cha wachezaji 16 ya wachezaji wa nyumbani kuanza matayarisho ya mashindano ya mwaka huu ya African Basketball Championships.

    Mashindano ya mwaka huu ya wanaume ya bara Afrika yameratibiwa kufanyika kuanzia Septemba 6 hadi 16 nchini Senegal na Tunisia. Kampuni ya Star Times imepewa kibali kupeperusha mashindano hayo rasmi.

    Rwanda ilijikatia tikiti kuingia mashindano hayo na FIBA Africa baada ya kushindwa kufuzu moja kwa moja kutoka mashindano ya Zone V Championship yaliyofanyika Misri mapema mwaka huu.

    Timu hiyo sasa imepangiwa kuanza mazoezi rasmi siku ya Jumatatu kwenye uwanja wa Amahoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako