• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu waongezeka kwa asilimia 46

  (GMT+08:00) 2017-08-03 17:10:46

  Takwimu zilizotolewa leo na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, biashara kati ya China na Afrika inaongezeka, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili katika nusu ya kwanza ya mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 19. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, uchumi wa Afrika umeonesha hali ya kufufuka. Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa imekadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa Afrika kwa mwaka huu litafikia asilimia 3.2, na kuongezeka kwa asilimia 1.7 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing, msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, China na Afrika zimeharakisha utekelezaji wa Mipango kumi ya Ushirikiano kati yao kwenye sekta za kilimo, viwanda, miundo mbinu na mambo ya kifedha, hivyo biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

  Bw. Gao amesema, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Afrika imefikia dola za kimarekani bilioni 85.3, na kuongezeka kwa asilimia 19. Na thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika nchini China imefikia dola za kimarekani bilioni 38.4, na kuongezeka kwa asilimia 46.

  Bw. Gao amesema, kwenye bidhaa zilizoagizwa na China kutoka Afrika, thamani ya uagizaji wa matunda na kahawa imeongezeka kwa asilimia 151 na 77. Na vyombo vya mawasiliano vinavyotengenezwa na China vimekaribishwa na nchi za Afrika, uuzaji wa meli, magari na vifaa vya safari ya anga ya juu barani Afrika vimeongezeka kwa asilimia 200,161, na 252.

  Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kampuni za China barani Afrika umefikia dola za kimarekani bilioni 1.6, na kuongezeka kwa asilimia 22. Thamani ya uwekezaji wa China nchini Ethiopia, Zambia, Kenya na Djibouti imezidi dola za kimarekani milioni 100.

  Bw. Gao amesema miradi mikubwa ya ushirikiano kati ya China na Afrika inaendelezwa hatua kwa hatua. Reli ya Mombasa-Nairobi ilizinduliwa rasmi mwezi Mei. Machimbo ya uranium yanayoendeshwa na kampuni ya China nchini Namibia, yatachukua nafasi ya pili duniani kwa kuzalisha uranium nyingi. Eneo la viwanda linalojengwa kwa pamoja na mkoa wa Hunan nchini China na Ethiopia liko tayari kuzinduliwa, na baadhi ya kampuni kubwa za China zitaingia kwenye eneo hilo na kuwekeza. Imefahamika kuwa China pia itachukua hatua nyingi ili kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako