• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yazitaka pande husika kutimiza peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia

  (GMT+08:00) 2017-08-03 19:14:15

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema usalama ni kiini cha suala la nyuklia la peninsula ya Korea, na China inatarajia pande husika zitafuatilia usalama wa peninsula hiyo kupitia mazungumzo yenye usawa, na kutimiza hali ya kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea.

  Wang amesema hayo baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Bw. Mevlut Cavusoglu. Amesema China inapinga Korea Kaskazini kukiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kufanya tena majaribio ya makombora, pia inazitaka pande husika zisifanye hatua yoyote itakayosababisha hali kuzidi kuwa mbaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako