• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:wafanyikazi wa shirika la reli la Uganda wagoma

    (GMT+08:00) 2017-08-03 19:18:14

    Zaidi ya wafanyikazi 400 wa shirika la Rift Valley Railway la Uganda wamejiunga na mgomo kufuatia nyongeza ya mshahara na ukosefu wa mishahara ya miezi 2.

    Mgomo huo ulioanza mwezi uliopita na wafanyikazi kiasi sasa umekwamisha shughuli zote za usafiri wa reli hiyo.

    Abiria katika vituo vya Jinja,Kampala,Bubesembatia na tororo wote wamelazimika kutumia uchukuzi mbadala.

    Katibu mkuu wa shirika hilo Uganda Victor Byemaro amesema wafanyikazi hao wamejiunga na mgomo huo baada ya kukosa mishahara yao kwa miezi 2 kufuatia tofauti za usimamizi.

    Aidha swala la bima ya usalama pia limezua minunguniko miongoni mwa wahudumu hao waliosema bima bora itakayolipwa na shirika hilo.

    Isiah Okoth mkurugenzi mkuu wa shirika hilo amekanusha uhalali wa mgomo huo akisistiza wahudumu wao hawakutoa rasmi agizo hilo kwa muungano wao..

    Reli hii inasimamiwa na Kenya na ushirikiano na Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako