• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Uber kutoa huduma ya bure kwa walemavu na wazee siku ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-08-03 19:19:24

    Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imeshirikiana na kampuni ya uchukuzi ya taxi Uber kuwapatia huduma ya bure walemavu na wazee katika siku ya uchaguzi mkuu.

    Loic Amado meneja mkuu wa Uber Afrika Mashariki ,amesema kwamba wamepewa majina na nambari za simu za walengwa hao na watahakikisha wamewafikisha katika vituo vya kupiga kura kama walivyoagizwa.

    Aidha Amado ameahidi pia kutoa diskaunti ya shilingi 200 kwa kila mteja atakaetumia huduma yao wakati wa uchaguzi.

    Kwa mujibu meneja huyu,ushurikiano huu unahimiza wakenya kufika katika vituo vya kura na kushiriki katika zoezi la kupiga kura ya kuchagua rais na viongozi wengine.

    Mradi huu umepewa jina la vote 2017 .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako