• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kenya yajiweka katika nafasi bora ya utalii wa kikanda

    (GMT+08:00) 2017-08-03 19:20:24

    Kenya inaendelea kujipatia nafasi kama kituo bora cha wageni kutoka nchi za kanda ya Afrika Mashariki kwa ajili ya shughuli za sherehe,hafla za kifamilia na sherehe za ndoa na fungate.

    Haya yamethibitishwa na bodi ya kitaifa ya utalii iliyoripoti ongezeko la wageni kutoka nchi za Afrika mashariki kuwasili katika hoteli na kumbi la mikutano.

    Bodi ya utalii sasa imeshirikiana na shirika la kupanga ratiba za maonyesho ya utalii wa Kenya kuandaa kituo maalum cha wanandoa kuzuru kwa likizo ama fungate.

    Hii ni baada ya kundi moja la Uganda Vision kufanya maonyesho ya siku tatu ya harusi za kitamaduni za Uganda hapa nchini Kenya.

    Mwaka jana Kenya iliandikisha jumla ya wageni 52,023 kutoka Uganda baada ya kushirikiana msanii wa muziki Edy Kenzo akiwa balozi wa utalii wa Kenya Uganda.

    Katika maonyesho hayo ya siku tatu zaidi ya watalii elfu 8 walihudhuria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako