• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa maoni kuhusu jeshi la India kuingia ardhi ya China

    (GMT+08:00) 2017-08-03 20:52:00

    China imetoa waraka wa "ukweli kuhusu kikosi cha ulinzi wa mpakani cha India kuingia ardhi ya China katika eneo la Sikkim la mpaka kati ya China na India na msimamo wa China".

    Ikijibu waraka huo, wizara ya mambo ya nje ya India imesema amani na utulivu wa eneo la mpakani kati ya India na China ni msingi wa maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Akizungumzia suala hilo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Geng Shuang amesema ingawa sasa India inazungumzia amani, ni vema vitendo vikafuatiliwa zaidi kuliko maneno. Amesema tangu mwezi June, askari wa India walivuka mpaka na kuingia kwenye ardhi ya China, na mpaka sasa askari hao bado wapo kwenye ardhi ya China. Amesema kitendo cha India kamwe hakilengi amani, na kwamba kama India kweli inathamini amani, inatakiwa kurudisha askari wake mara moja kwenye ardhi ya India.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako