• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wladmir Klitschko amkimbia Anthony Joshua kwa kuamua kustaafu ndondi

    (GMT+08:00) 2017-08-04 09:12:40
    Aliyekuwa bingwa wa dunia katika ndondi Wladmir Klitschko amestaafu ndondi na kupelekea kufutiliwa mbali uwezekano wowote wa mechi ya marudiano dhidi ya Anthony Joshua.

    Raia huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41 alipigwa knockout katika raundi ya 11 na bingwa wa sasa Joshua katika uwanja wa Wembley mwezi Aprili .

    Taarifa toka Ujerumani zinasema Klistcho mwenye miaka 41 ameamua kuachana na mchezo huo aliodumu nao kwa miaka 21 na hivyo kusimamisha ndoto za wapenda masumbwi kumuona akipigana tena na Joshua.

    Joshua mwenye umri wa miaka 27 alitumai kwamba Klitschko atashiriki mechi ya marudiano mjini Las Vegas Novemba 11.

    Klitschko maarufu kama Dr Steelhammer ambaye ni bingwa mara mbili wa uzani mzito dunia ameshacheza mapambano 69 hadi hivi sasa, akiwa ameshinda mara 64 na kushindwa mara 5.

    Klistcho ameshawahi kushinda mataji makubwa ya masumbwi duniani ikiwemo IBF, WBO, WBA na IBO na taji lake kubwa la kwanza alishinda mwaka 1992 baada ya kumtwanga Marcus Mclntyre.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako