• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaapa kuendeleza ushindi katika mbio za Dunia mjini London

    (GMT+08:00) 2017-08-04 09:13:40

    Riadha za Dunia zitatimua vumbi leo usiku, huku mabingwa watetezi Kenya wakisaka mwanzo mzuri wakati mfalme wa kilomita 21 Geoffrey Kamworor, malkia wa mita 1500 Faith Chepng'etich na nyota wa mbio fupi Mark Otieno watashuka uwanjani Olympic jijini London.

    Otieno atakuwa Mkenya wa kwanza kutimka. Atapeperusha bendera ya Kenya pekee yake katika mbio za mita 100 na mita 200.

    Mkimbiaji huyu mwenye umri wa miaka 24 anajivunia muda wa kasi ya juu mwaka 2017 katika kundi lake la mchujo.

    Otieno atamenyana na wanariadha mbalimbali wakiwemo Emmanuel Matadi wa Liberia, Brendon Rodney wa Canada na Masbah Ahmed wa Bangladesh. Awamu hii ni ya kuingia raundi ya kwanza. Nao Chepng'etich, Judy Kiyeng' na Winny Chebet watakuwa mawindoni uwanjani katika mbio za mizunguko mitatu.

    Wakenya wameapa kumaliza utawala wa Farah, lakini lazima pia wawe macho kabisa na wakimbiaji kutoka Ethiopia, ambao wana muda mzuri sana.

    Kenya iliibuka bingwa wa dunia mwaka 2015 iliponyakua medali saba za dhahabu, sita za fedha na tatu za shaba hapa mjini Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako