• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Palestina yalaani waziri mkuu wa Israel kwa kushiriki kwenye uzinduzi wa mradi wa makazi mapya ya Wayahudi

  (GMT+08:00) 2017-08-04 10:07:50

  Ikulu ya Palestina imetoa taarifa ikimlaani waziri mkuu wa Israel Bw Benjamin Netanyahu kushiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la makazi mapya ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi, kitendo ambacho Palestina inasema kinahujumu Mpango wa nchi mbili.

  Msemaji wa ikulu ya Palestina Bw Rudeineh amesema maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza ni ardhi ya Palestina inayokaliwa, ujenzi wa makazi ya Wayahudi kwenye maeneo hayo ni haramu, na kinaharibu maslahi ya watu wa Palestina.

  Bw Rudeineh ameilaani serikali ya Israel kwa kuvuruga juhudi za rais Donald Trump wa Marekani kuanzisha tena mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel, na kutoa wito kwa Marekani iizuie Israel kupanua makazi ya Wayahudi kwenye ardhi ya Palestina.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako