• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wizara ya ulinzi ya China yaitaka India iondoe mara moja vikosi vyake kutoka ardhi ya China

  (GMT+08:00) 2017-08-04 10:26:40

  Wizara ya ulinzi ya China imeitaka India iondoe mara moja vikosi vyake vilivyovuka mpaka na kuingia China.

  Kwenye taarifa iliyotolewa jana usiku kwenye tovuti ya wizara ya ulinzi ya China, msemaji wa wizara hiyo Bw. Ren Guoqiang amesema tangu kutokea kwa tukio hilo, China imeonyesha nia njema na kujitahidi kutafuta njia za kidiplomasia ili kutatua suala hilo. Amesema Jeshi la China pia limeonyesha uvumilivu kwa ajili ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na amani na utulivu wa kikanda.

  Amesisitiza kuwa nchi yoyote haipaswi kutweza imani na uwezo wa jeshi la China katika kulinda amani, na wala haipaswi kutweza dhamira na nia ya jeshi la China katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako