• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuanza safari za moja kwa moja kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-08-04 20:01:31

    Ndoto ya Kenya kuanza safari za ndege za moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani huenda ikatimia ifikapo Disemba mwaka huu.Hii ni baada ya Kenya kuweka mfumo kuangalia hali ya hewa ikiwa ni mojawapo ya matakwa ya serikali ya Marekani.Akizungumza na radio China Kimataifa baada ya kushuhudiwa kuwekwa kwa mfumo huo katika uwanja wa ndege, waziri wa mazingira wa Kenya bi Judy Wakhungu amesema mfumo huo umewekwa kwa gharama ya shilingi milioni 200. Mfumo huo unakagua mkondo wa mawimbi, hali joto, dhoruba miongoni mwa mambo mengine yanayohusiana na hali ya hewa. Mfumo huo utakuwa ukitoa matokeo kila baada ya dakika 10. Wakhungu ameongeza kuwa safari za moja kwa moja zitasaidia kuinua hadhi ya Kenya katika jukwaa la kimataifa. Taarifa hii inakuja miezi michache tu baada ya shirika la ndege la Kenya kuomba kibali cha kufanya safari za moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako