• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yaanza mchakato wa kuvichukua viwanda vilivyoshindwa kutimiwa wajibu wa uzalishaji

    (GMT+08:00) 2017-08-04 20:02:11

    Serikali ya Tanzania imesema viwanda inavyochukua ni vile vilivyoshindwa kutimiza wajibu wa uzalishaji na kuongeza ajira nchini humo.

    Katibu mkuu katika wizara ya viwanda, Biashara na uwekezaji, Bw Adelhelm Meru amesema hatua hiyo haina ubaya hata kidogo kwa kuwa inalenga kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Tanzania. Kauli hiyo inakuja muda mfupi tu baada ya baadhi ya wanasiasa nchini humo kupinga hatua hiyo ya serikali. madai ya

    Baadhi ya viwanda ambavyo vimenyakuliwa ni pamoja na Pipeline Industries, Global Packaging, Masasi Food Industries, CATA Mining Ltd. Aidha Bw Meru amesema katika kipindi hiki, jumla ya viwanda vilivyosajiliwa na kuanza utekelezaji kupitia TIC ni 224, kupitia EPZA ni 41 na kupitia BRELA ni 128 na kuongeza kuwa jumla ya viwanda vidogo na vya kati vilivyoanzisha na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ni 2,243.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako