• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yashinda tenda ya ujenzi wa jengo la maofisi ya serikali

    (GMT+08:00) 2017-08-04 20:02:37

    Kampuni ya China imefanikiwa kushinda tenda ya shilingi bilioni 3.1 ya ujenzi wa jengo la maofisi mjini Nairobi. Kampuni hiyo kwa jina Aviation Industry Corporation inatarajiwa kutekeleza mradi huo ambao unafadhiliwa na benki ya dunia. Jengo hilo linatarajiwa kuwa makao ya ofisi nyingi za serikali ya Kenya. Miradi mingine ambayo inaendeshwa na kampuni hiyo ya China ni pamoja na mradi wa shilingi bilioni 20 wa ujenzi wa jengo kubwa na refu zaidi barani Afrika katika eneo la Westlands mjini Nairobi.Wakati huo huo serikali imewataka wawekezaji pamoja na wafanya biashara kuondoa wasiwasi kuhusu usalama wao wakati huu ambapo Kenya inajiandaa kufanya uchaguzi wiki ijayo. Taarifa hii inakuja wakati ambapo baadhi ya wawekezaji wamekuiwa na hofu ya kutokea kwa fujo ambazo huenda zikaharibu biashara zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako