• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watanzania kutumia simu ya mkononi kulipia kodi ya ardhi

  (GMT+08:00) 2017-08-04 20:03:05

  Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Tanzania imeanzisha rasmi mfumo mpya wa kulipia kodi ya ardhi kwa njia ya kieletroniki, unaolenga kupunguza kero wanazopata walipa kodi ya kutumia muda na mlolongo mrefu wakati wa kulipia.

  Kuanzia sasa, mmiliki yeyote mwenye ardhi iliyopimwa na kupatiwa hati ya umiliki, anaweza kuulizia kiasi cha fedha anazodaiwa na kulipia kodi hiyo ya mwaka kwa kutumia simu yake ya mkononi, tovuti ya wizara hiyo au kulipia kupitia benki. Pamoja na hayo, wizara hiyo imepanga kushirikiana na serikali za mitaa kufanya ukaguzi maalumu wa maeneo yote ya ardhi yasiyopimwa, ili kujua ni wananchi wangapi wana maeneo hayo na maeneo gani, waweze kuingizwa kwenye mfumo wa kulipia kodi ya ardhi.

  Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Moses Kusikula amesema mfumo huo utamuwezesha mmiliki wa ardhi kulipia ardhi hiyo kwa dakika chache, badala ya kutumia siku nzima kusubiri kupata huduma ya malipo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako