• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Kichina yaanza ukarabati wa uwanja wa Namfua, TZ

    (GMT+08:00) 2017-08-07 10:39:05
    Kampuni ya Kichina, China Sichuan International Cooperation Co Ltd (SIETCO) imejitolea kusaidia juhudi za kurekebisha Uwanja wa michezo ya Namfua jijini Dar es Salaam, ili kuuwezesha uwanja huo tayari kwa ajili ya Ligi kuu ya bara.

    Uwanja wa Namfua ni nyumbani mwa klabu iliyopandishwa daraja Singida United, ambayo ilirudi kwenye daraja la juu msimu huu baada ya kuwa nje kwa karibu misimu tano. Ligi imeratibiwa kuanza rasmi Agosti 26 mwaka huu.

    Afisa mmoja wa kampuni ya SIETCO, Tan Jian alisema walikubaliana kutoa msaada huo baada ya wamiliki wa Uwanja, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Singida kutuma maombi.

    Tan alisema baadhi ya shughuli inayofanyika katika uwanja huo ni pamoja na kusafisha eneo lote linalozunguka uwanja, kusawazisha na kukusanya uchafu wote na takataka kwa sehemu ya utupaji ili kupea uwanja huo sura mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako