• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Team Rwanda tayari kwa mashindano ya Colorado Classic

    (GMT+08:00) 2017-08-07 10:39:41
    Timu ya kitaifa baiskeli ya Rwanda, maarufu kama Team Rwanda, imeongeza maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya Colorado Classic yaliopangwa kufanyika Agosti 10-13 Marekani.

    Kwa mujibu wa kocha mkuu, Sterling Magnell, Jean Claude Uwizeye aliyejeruhiwa wakati wa mashindano ya Cascade Cycling Classic, amepona na atakuwa tayari kwa mchezo wa kitengo cha HC UCI yenye hatua nne itakayomaliza umbali wa jumla ya kilomita 503.5

    Timu hiyo yenye wanabaiskeli sita ikiongozwa na Magnell na msaidizi wake Felix Sempoma, imekuwa Marekani tangu Julai 14 ambapo walishiriki katika mashindano ya Cascade Classic Julai 19-23.

    Hapo jana Magnell alifichua kuwa wanabaiskeli hao wanafanya vizuri katika mazoezi na kwamba wamepata masomo muhimu kutoka mashindano ya Cascade Classic na yatakuwa ya manufaa katika mashindano hayo ya Colorado Classic wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako