• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yamaliza katika nambari ya tatu raga ya Afrika

    (GMT+08:00) 2017-08-07 10:39:57
    Uganda imemaliza Raga ya Afrika (Africa Gold Cup) katika nafasi ya tatu baada ya kunyamazisha Zimbabwe kwa alama 38-12 jijini Kampala katika mechi yake ya mwisho wikendi hii.

    Namibia ilitawazwa mabingwa kwa kulaza Kenya 45-7 jijini Windhoek mwishoni mwa mwezi uliopita. Mabingwa mara saba Namibia walimaliza makala ya mwaka huu wa 2017 kwa pointi 25 nao mabingwa wa mwaka 2011 na 2013 Kenya wakafunga mashindano katika nafasi ya pili kwa pointi 16.

    Uganda pia imemaliza mashindano haya ya mataifa sita kwa pointi 16. Kenya imeishinda Uganda kwa ubora wa pointi. Ilifunga pointi 226 na kufungwa 135 nayo Uganda ilimaliza na 190-126.

    Mabingwa wa mwaka 2012 Zimbabwe wanasubiri matokeo ya mechi kati ya Tunisia na Senegal kujua watamaliza katika nafasi ya nne ama tano. Wazimbabwe, ambao wanashikilia nafasi ya nne, wamekamilisha mechi zao tano kwa pointi sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako