• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Faith Chepng'etich ashindia Kenya dhahabu mbio za mita 1500

    (GMT+08:00) 2017-08-08 10:18:41

    Bingwa wa olimpiki katika mbio za mita 1,500 Faith Chepng'etich aliongeza medali nyingine katika kabati lake aliponyakulia Kenya taji lake la kwanza la dhahabu katika mbio za wanawake za dunia za mita 1,500 katika uwanja wa Olympic jijini London Jumatatu.

    Chepng'etich aliyeandikisha historia alikimbia mbio za kufana japo kwa kiufundi alipompiku mwanariadha kutoka Uholanzi Sifan Hassan kabla ya mkimbio wa mwisho na kushinda kwa dakika 4 sekunde 02.59.

    Chepng'etich, alimshinda mwanariadha kutoka Marekani Jenniffer Simpson aliyejinyakulia medali ya fedha na bingwa wa olimpiki katika mbio za mita 800 Caster Semenya kutoka Afrika Kusini aliyeshinda shaba.

    Ilikuwa mbio za kufana na yenye mafanikio kwa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye alishinda medali ya fedha katika mashindano ya dunia ya mwaka 2015 jijini BeIjing, baada ya kumaliza wa tano katika mashindano ya dunia ya Moscow mwaka 2013 alipoanza kukimbia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako