• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yashinda Sudan ikisubiri mchuano na Uganda

    (GMT+08:00) 2017-08-08 10:19:06

    Timu ya taifa ya soka ya Rwanda, Amavubi, ilishinda Sudan 2-1 katika mechi ya kirafiki katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali siku ya jumatatu.

    Washambuliaji wa klabu ya AS Kigali Dominic Nshuti Savio na Bernabe Mubumbyi walifungia mabao timu hiyo ya nyumbani ilihali Saifedin Maki akafunga bao la Sudan.

    Pande zote mbili zilikuwa zikitumia mechi hiyo kama matayarisho kwa michuano yao kufuzu kombe la mashindano ya Afrika CHAN 2018.

    Timu hiyo inayoongozwa na kocha Antoine Hey ilianza vyema na ikachukua uongozi katika dakika ya 3 wakati chipukizi Kevin Muhire na Emmanuel Imanishimwe waliunganisha mchezo wao na kumpa nafasi kijana Nshuti, aliyefunga dhidi ya Tanzania katika raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu.

    Rwanda itasafiri kuelekea Uganda hapo kesho ambapo itachuana na timu ya soka ya taifa Uganda Cranes siku ya Jumamosi kwa mkumbo wa kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako