• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makampuni ya kibinafsi ya kuzalisha sukari yapewa leseni za kuagiza sukari kutoka nje

  (GMT+08:00) 2017-08-08 19:25:23

  Mamlaka ya Kilimo na Chakula nchini Kenya imetoa kibali cha kuagiza sukari bila kulipa kodi kwa makampuni ya kibinafsi ya Kenya. Serikali inatarajia makampuni hayo kuagiza tani elfu 150 za sukari. Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kilimo na chakula ya Kenya Bwana Alfred Busolo amesema hatua hiyo inalenga kuyawezesha makampuni ya sukari kuwa na hifadhi ya kutosha ya sukari katika maghala yao ili wananchi wasikose bidhaa hiyo muhimu. Aidha wafanyabiashara hao wametakiwa kuweka maelezo kuhusu mahali sukari inakotoka wakati wanapowauzia wateja. Bidhaa hiyo inatarajiwa kuanza kuwasili katika bandari ya Mombasa baada ya mwezi mmoja.Kenya inashuhudia upungufu wa tani milioni 1.9 za sukari kufuatia ukame ambao umeshuhudiwa katika maeneo yanayokuza miwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako