• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania kutangaza kodi mpya ya ardhi

  (GMT+08:00) 2017-08-08 19:25:40

  Serikali ya Tanzania imesema kuanzia mwaka huu itatangaza kodi ambayo watu wote wenye viwanja nchini humo, wakiwemo wanaoishi katika makazi yasiyopimwa, wataanza kulipa kodi hiyo ya ardhi kwa kuhakikisha wananchi wote wanaishi katika makazi yaliyorasimishwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari, waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Bwana William Lukuvi amesema wanaoishi katika makazi yasiyopimwa watatambuliwa kwa kupewa leseni za makazi zitakazokuwa na ukomo na kutakiwa kuishi kwa muda utakaopangwa na baada ya kipindi hicho kumalizika, watatakiwa maeneo yao yawe yameshapimwa tofauti na hivyo manispaa zitaagizwa kufunga nyumba zao.

  Aidha, amesema serikali haitojihusisha tena katika kupima maeneo yoyote ya ardhi kuanzia sasa, na badala yake kinachotakiwa ni wananchi wenyewe kuwajibika kwa kuunda kamati za urasimishaji zitakazosaidia maeneo yao kupimwa.

  Kadhalika serikali imesema katika kudhibiti matapeli wa ardhi, na migogoro mbalimbali ya ardhi, itaanzisha mradi mpya utakaoanzia katika Manispaa ya Ubungo na Kinondoni nchini humo ambao utawezesha kutoa hati za makazi katika njia ya elektroniki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako