• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara zasimama huku wakenya wakijitokeza kwa wingi kupiga kura

  (GMT+08:00) 2017-08-08 19:26:01

  Biashara leo zilisimama nchini Kenya baada ya wafanya biashara kufunga biashara zao ili kutoa nafasi kwa wakenya kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupiga kura kuwachagua viongozi wao. Katika mji mkuu wa Nairobi, maduka yalionekana kufungwa huku milolongo mirefu ikishuhudiwa katika vituo mbali mbali vya kupigia kura. Baadhi ya wafanya biashara waliozungumza na radio China Kimataifa, wamesema waliamua kuchukua hatua hiyo ili kuwawezesha wakenya kutimiza haki zao za kikatiba. Hata hivyo wachuuzi wa kahawa walionekana wakifurahia biashara baada ya kuwauzia wapiga kura ambao walikuwa wakipiga foleni kusubiri nafasi yao. Baadhi yao walisema kahawa imewasaidia sana katika kukabiliana na baridi kali wakati wa asubuhi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako