• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu saba wamefariki dunia baada ya tetemeko lenye nguvu ya 7 kwenye kipimo cha Ritchter kutokea kusini magharibi mwa China

  (GMT+08:00) 2017-08-09 08:37:27

  Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7 kwenye kipimo cha Richter limeikumba sehemu ya ndani ya mkoa wa Sichuan, ulioko magharibi mwa China, na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine 164 kujeruhiwa.

  Kituo cha kufuatilia matetemeko cha China kimesema kiini cha tetemeko hilo lililotokea jana saa tatu usiku katika kivutio maarufu cha watalii cha Jiuzhaigou, kwenye kina cha kilomita 20 kutoka ardhini.

  Rais Xi Jinping na Waziri Mkuu Bw Li Keqiang wametoa maagizo kwa idara za huko kufanya kila linalowezekana na kuwasaidia majeruhi.

  Watalii elfu 34 walitembelea kivutio cha Jiuzhaigou hapo jana, watu 100 walikwama katika nyumba moja kutokana na maporomoko ya udongo, lakini hakuna aliyejeruhiwa.

  Habari pia zinasema tetemeko lenye nguvu ya 6.6 limetokea mkoani Xinjiang asubuhi ya leo, mpaka sasa hakuna habari kuhusu wahanga au hasara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako