• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msukosuko wa kibinadamu wa Mosul Iraq bado kwisha

  (GMT+08:00) 2017-08-09 08:37:55

  Msukosuko wa kibinadamu wa Mosul Iraq bado kwisha

  Mratibu wa maswala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Bibi Lisa Grande amesema hali ya kibinadamu nchini Iraq inaendelea kuwa mbaya, wakati serikali ikiendelea na kazi ya kuwahamisha watu kabla ya hatua za mwisho kuliondoa kundi la IS.

  Bibi Grande amesema licha ya kuwa Syria inabaki kuwa na operesheni kubwa zaidi za mambo ya kibinadamu, watu wengine nchini Iraq wanapoteza makazi yao kwa kasi zaidi kuliko sehemu yoyote duniani. Ametolea mfano wa Mji wa Mosul ambao amesema licha ya kuondolewa kwa kundi la IS msukosuko wa kibinadamu bado unaendelea, na watu zaidi wanatarajiwa kupoteza makazi yao, baada ya kuanza kwa operesheni nyingine dhidi ya wapiganaji wa kundi la IS katika mji wa Tal Afar karibu na Mosul.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako