Bunge la Afrika Kusini limepiga kura ya siri kuhusu kukosa imani na rais Jacob Zuma, ikiwa ni mara ya nane kupigiwa kura hiyo. Kutokana na kura hizo kutofikia zaidi ya nusu ya wabunge, mswada huo haukupitishwa
Spika wa bunge Bibi Baleka Mbete, amesema kati ya wabunge 384 waliopiga kura, wabunge 198 walipiga kura ya kupinga mswada huo, wengine 177 walipiga kura ya kuunga mkono mswada huo, na wabunge 9 waliacha kupiga kura.
Baada ya upigaji kura huo, chama tawala cha ANC kimetoa taarifa kikisema, licha ya kuwa kuna masuala mengi nchini Afrika Kusini, lakini mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa chama hicho hayawezi kukanushwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |