• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waraka wa ulinzi wa Japan wa mwaka 2017 walipaka matope jeshi la China

  (GMT+08:00) 2017-08-09 09:49:13

  Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema mambo yaliyomo kwenye waraka wa ulinzi wa Japan uliotolewa jana yanalipaka matope jeshi la China kwa nia mbaya na kudanganya jumuiya ya kimataifa. Jeshi la China limepinga kithabiti waraka huo.

  Bw. Wu Qian amesema Japan inatetea kuwa China inataka kubadilisha hali ya bahari ya mashariki na bahari ya kusini, ambayo imekuwa wasiwasi wa pamoja wa kimataifa na wa kikanda, lakini hali halisi ni kwamba Japan inajaribu kubadilisha hali hiyo na kusababisha wasiwasi wa jumuiya ya kimataifa.

  Bw. Wu Qian ameongeza kuwa, Japan pia inasema uwongo na kulaumu mwelekeo wa maendeleo ya jeshi la China. China inashikilia kutekeleza sera ya ulinzi ya kujilinda na mkakati wa kijeshi wa kujilinda, inapanua mawasiliano ya kijeshi, kushiriki kwenye operesheni za kulinda amani, kulinda usalama wa meli na kutoa uokoaji wa kibinadamu, ambazo zimeonyesha sura nzuri za jeshi la nchi linalobeba majukumu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako