• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Conseslus Kipruto ashinda dhahabu mbio za kuruka viunzi na maji

  (GMT+08:00) 2017-08-09 10:25:48
  Bingwa wa Olimpiki Conseslus Kipruto alidumisha ubabe wa Kenya katika mbio za mita 3,000 kuruka maji na viunzi, na kunyakulia nchi hiyo taji la dunia kwa mbio hizo kwa mara sita mtawalia katika uwanja wa Olimpiki ya London jumanne Usiku.

  Mwamerika Evan Jager alichukua uongozi baada ya mita 2,000 huku Kipruto, bingwa mtetezi Ezekiel Kemboi na mwanariadha kutoka Morocco Souffiane Elbakkali wakiwa nyuma.

  Jager, ambaye ni mshindi wa medali ya Fedha katika mbio hizo, alikuwa kifua mbele katika mzunguko wa mwisho lakini Kipruto akaongeza kasi na kutwaa uongozi katika mita za mwisho.

  Mkenya huyo aliyekuwa ameshinda medali za fedha katika mashindano ya dunia ya mwaka 2013 na 2015, alikuwa na fursa ya kutania mashabiki waliokuwa wamejaa uwanjani kabla ya kushinda mbio hizo kwa dakika 8:14.12. Elbakkali wa Morocco alinda Fedha naye Jager akapata medali ya shaba baada ya kumaliza wa tatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako