• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba yalaza Rayon Sports ya Rwanda, Simba Day

  (GMT+08:00) 2017-08-09 10:26:28
  Haruna Niyonzima ameanza vyema kibarua chake kipya baada ya kuiongoza Simba kuibuka na ushindi, na kuonyesha kiwango cha kuvutia

  Kikosi cha Simba kiliadhimisha vyema tamasha la kutambulisha wachezaji wake wapya pamoja na kuzindua jezi mpya itakazo tumia kwenye msimu unaokuja, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda.

  Katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kiungo wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima aliichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo na kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

  Mohamed Ibrahim 'MO' aliifungia Simba bao la mapema dakika ya 16, baada ya kupokea pasi nzuri ya Emmanuel Okwi ambaye naye kabla ya kutoa pasi hiyo aliwalamba chenga walinzi wa Rayon Sport.

  Rayon ambao ni mabingwa wa Rwanda, walionyesha kiwango cha hali ya chini na kuwaacha wenyeji Simba, kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi lakini washambuliaji John Bocco na Okwi walishindwa kuzitumia vizuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako