• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Karia, Mulamu waahidi mabadiliko shirikisho la TFF

  (GMT+08:00) 2017-08-09 10:26:50
  Wawaniaji wanaogombea nyadhifa za ngazi za juu katika uchaguzi ujao wa shirikisho la kandanda Tanzania TFF walizindua kampeini zao jana kwa mbembwe, wakiahidi mabadiliko makubwa katika shirikisho hilo.

  Rais wa mpito wa shirikisho hilo Wallace Karia amesema ataangazia uwazi, uwajibikaji, uaminifu na ,maendeleo ilihali Mulamu Nghambi, anayewania kiti cha makamu wa rais akidumisha kwamba atapigania utendakazi bora katika masuala ya usimamizi wa soka.

  Punde tu baada ya kupata kibali kuwania nafasi katika shirikisho hilo, Karia aliitisha mkutano na vyombo vya habari katika uwanja wa taifa Dar es Salaam ambapo aliwaakikishia umma kwamba miaka aliyotumikia TFF imempa uzoefu na kumwezesha kujifunza mengi yatakayomwezesha kuleta mabadiliko katika shirikisho hilo na kuimarisha mchezo wa kandanda Tanzania

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako