• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid yanyakua Kombe la Uefa Super Cup

    (GMT+08:00) 2017-08-09 10:27:27
    Mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid walizidi nguvu Manchester United ya Uingereza kwenye mechi ya Kombe la UEFA Super Cup iliyochezwa Macedonia.

    Madrid walidhibiti mchezo huo kuanzia kipenga cha kwanza na kwa haraka wakajipata kifua mbele pale Casemiro alipowafungia bao, muda mfupi baada ya kugonga mwamba wa goli.

    Waliongeza la pili kupitia Isco aliyefunga akiwa hatua nane kutoka kwenye goli baada ya kubadilishana pasi na Gareth Bale, ambaye alichezeshwa safu ya mashambulizi badala ya Cristiano Ronaldo.

    Mshambuliaji wa United Romelu Lukaku, aliyenunuliwa milioni 75 pauni ya Uingereza, alikomboa bao moja lakini Marcus Rashford akapoteza fursa nzuri ya kufunga kwa kuutuma mpira nje.

    Madrid ni timu ya kwanza kufanikiwa kutetea Kombe la Super Cup la Uefa tangu 1990. Mechi hiyo ilichezwa chini ya joto kali la nyuzi joto 30 katika mji mkuu huo wa Macedonia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako