• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Macho ya kulinda msitu

    (GMT+08:00) 2017-08-09 18:02:15

    Kuzuia ajali ya moto ni muhimu zaidi kati ya kazi za kulinda misitu. Katika msitu wa Saihanba ulioko mkoani Hebei, China, ingawa mitambo ya kisasa kama vile rada ya kugundua moto na kamera za uchunguzi zimewekwa, lakini uchunguzi wa binadamu bado ni muhimu zaidi, na watu wa kuchunguza ajali ya moto wanajulikana kama macho ya kulinda misitu.

    Bw Liu Jun mwenye umri wa miaka 46 anafanya kazi ya kuchunguza ajali za moto katika msitu wa Saihanba. Yeye ni mfupi, na rangi ya ngozi zake ni nyeusi kutokana na kuchomwa na jua kwa muda mrefu. Anaongea polepole, lakini anapozungumzia msitu mkubwa anaolinda, anaweza kuongea kwa haraka kuhusu sehemu mbalimbali za misitu ambazo mtu wa kawaida hawezi kutambua tofauti hata kidogo. Mbali na kufahamu vizuri sehemu zote za msitu, Bw Liu Jun pia ana uwezo mkubwa wa kuona. Mtoto wake Liu Zhigang anayejifunza uwezo wa kuchunguza ajali ya moto anasema,

    "Siku moja nilifanya kazi na baba yangu. Kulikuwa na ukame, na kila likipita gari, vumbi litokea kama moshi. Nilidhani ajali ya moto ilitokea, lakini baba yangu alitupulia macho akiniambia ni vumbi tu."

    Katika msitu wa Saihanba, watu wanaoshughulikia kuchunguza ajali ya moto wanaheshimiwa na watu wengine, kwani kazi hiyo ni muhimu sana. Aidha, minara ya kuchunguza ajali ya moto huwa kwenye sehemu ya juu yenye watu wachache, na watu wanaofanya kazi katika minara hiyo wanavumilia upweke kwa muda mrefu. Hivyo ni vigumu kupata watu wanaopenda kazi hiyo. Ili kutatua tatizo la upweke, kati ya minara 9 ya kuchunguza ajali ya moto katika msitu wa Saihanba, wafanyakazi wa minara 8 ni wanandoa.

    Mwaka 2006, Bw Liu Jun na mke wake Qi Shuyan ambao walikuwa wafanyakazi wa kawaida wa msitu huo, walibadilisha kazi na kuanza kuchunguza ajali ya moto katika mnara mrefu zaidi msituni, ambako ni sehemu wazazi wa Bw. Liu Jun walipofanya kazi zamani.

    "Niliambiwa na mama yangu kuwa walifanya kazi hapa mpaka nilipofikisha umri wa miaka mitano. Nyumba yao ilikuwa kibanda. Hakukuwa na barabara, walitembea kwa miguu tu. Pia hakukuwa na miti mingi kama sasa, na upepo mkali ulirusha mchanga. Mama yangu aliniambia nilizaliwa hapa, na kuhama nilipokuwa mkubwa."

    Ingawa Bw. Liu Jun anafanya kazi na mke wake, lakini upweke bado ni changamoto kubwa zaidi inayowakabili. Baadhi ya wakati, wanabishana.

    "Ni nadra kuwakuta watu hapa, upweke unatusumbua. Baadhi ya wakati tunabishana bila sababu."

    Hadi sasa Bw Liu Jun na mke wake wamefanya kazi katika mnara huo kwa miaka 11. Katika kipindi cha miezi sita chenye ukame zaidi kila mwaka, mchana wanatoa ripoti kila baada ya dakika 15, na wakati wenye hatari zaidi, hata usiku wanatakiwa kutoa ripoti kila baada ya saa moja. Kazi ni ngumu, lakini wanashirikiana vizuri. Qi Shuyan anasema,

    "Katika kipindi chenye hatari ya ajali ya moto, anashika zamu ya usiku. Anapenda kuchelewa kulala. Hivyo nalala nusu ya kwanza ya usiku, na analala nusu ya pili. Wakati wa alfajiri naendelea na kazi yake, anaandaa kifungua kinywa, baada ya kula anashika zamu tena. Halafu baada ya kumaliza kazi ya usafi, narudi kazini tena. Tunafanya hivyo."

    Baada ya kufanya kazi msituni kwa muda mrefu, sasa hawazoei maisha ya mjini. Safari yao ya mwisho ya kwenda nyumbani kwao mjini ni mwezi Juni mwaka huu wakati wa ndoa ya mtoto wao. Kuhusu mtoto huyo Liu Zhigang, Bw Liu Jun na Qi Shuyan wana masikitiko moyoni. Kama wafanyakazi wengine wengi wa msitu, walimpeleka mtoto wao mjini alipokuwa na umri wa kusoma shuleni. Awali Liu Zhigang hakukubali kuishi mjini bila wazazi wake, lakini sasa ameelewa umuhimu wa kazi zao. Anasema,

    "Wakati wazazi wangu walipoanza kazi hapa, mimi nilikuwa mtoto mdogo. Miti ilikuwa midogo, na ilikuwa na urefu kama nusu ya mguu wangu. Kila nilipokuwa na likizo, nilikuja hapa na kuona miti inakua pole pole, sasa miti hiyo ni mirefu zaidi kuliko mimi. Nafurahi sana."

    Kazi na maisha magumu msituni vimewazesha kwa haraka Liu Jun na mke wake. Lakini wanaridhika sana. Matumaini yao ya hivi sasa ni kuwa baada ya kustaafu kwao, kuna watu wataendelea kulinda msitu huo. Bw Liu Zhigang anafahamu vizuri matumaini hayo ya wazazi wake, aliacha kazi ya kiwandani mjini Shanghai, na kuwa mzima moto wa msitu wa Saihanba. Katika kipindi kisicho na hatari ya moto, anaenda kwenye mnara na wazazi wake ili kujifunza uwezo wa kuchunguza ajali ya moto. Bw Liu Jun pia anatarajia kuwa kuna siku mtoto wake atashika jukumu lake la kulinda msitu huo. Anasema,

    "Baba yangu alianzisha kazi hapa, sisi ni kizazi cha pili, na mtoto wetu ni cha tatu. Hii ni kazi ya kurithi, tutaifanya vizuri."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako